Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Estim Construction Ltd, kuongeza kasi ya ujenzi na maboresho ya Soko la Kariakoo, ili likamilike kwa wakati.
Makalla ameyasema hayo katika wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa Soko lililoungua na Soko jipya lenye urefu wa gorofa sita, ambalo ujenzi unaghahirimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26.
Amesema, kukamilika kwa Soko hilo kutabadili mfumo wa uendeshaji biashara kwa kutoa wigo mpana wa kupokea Wafanyabiashara wengi toka 600 mpaka kufikia zaidi ya 2,000.
Kuhusu agizo la Rais Samia la kufanya biashara kwa saa 24, Mkuu huyo wa Mkoa amesema, kikosi kazi kinaendelea kufanya tathimini kisha kitawasilisha taarifa kwa ajili ya utekelezaji.
Hata hivyo, Makalla ameonyesha kuridhishwa na kasi ya Mkandarasi ambaye mpaka sasa amefikia asilimia 40 jambo linaloleta matumaini ya kukamilika kwa wakati kwa ujenzi wa soko hilo.