Mkandarasi anayetekeleza mradi wa REA 3 mzunguko wa pili ametakiwa kuongeza kasi ya kuunganisha umeme katika vijiji vyote Mkoani Kagera, vilivyoko katika mkataba kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko wakati akiwasha umeme katika Vijiji vya Ntanga na Kaburanzwili Wilaya ya Ngara, ambapo alisema kuwa katika awamu hiyo ya utekelezaji wa mradi wa REA mkoa wa Kagera umefikia asilimia 77 ya utekelezaji na hakuna kijiji kitakachobaki kila kijiji kitapata umeme.

Amesema, “Umeme ni uchumi, naamini kupitia umeme huu wananchi mtanufaika vya kutosha katika kuhakikisha mnaanzisha biashara zenu, mkaingize kipato katika familia zenu, lakini pia nimuombe mkandarasi kuongeza kasi ya kusambaza umeme katika vijiji vyote kwa sababu serikali haina changamoto ya fedha, fedha ipo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba Ruhoro amesema uwepo wa umeme utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi, huku akisema kwa muda mfupi ambao umeme umeanza kuwaka vijijini tayari shughuli za kiuchumi zimeongezeka.

Wengi wajitokeza uchunguzi wa Saratani, Wanawake wapewa neno
Wavuvi, Wafugaji, Wakulima wawezeshwa zana za kazi