Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Angela Kairuki ametangaza nafasi za ajira 21,200 kwa kada za walimu na afya, ambazo maombi yake yanaanzia leo hadi April 25,2023.

Waziri Kairuki ametangaza ajira hizo hii leo Aprili 12, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma na kutaja mgawanyo wa nafasi hizo kuwa ni afya yenye nafasi 8,070 kwa watumishi wa ngazi ya zahanati, vituo vya afya na Hopsitali na walimu wa shule za msingi na Sekondari nafasi 13,130.

Amesema, “Rais ametoa kibali cha kuajiri watumishi nasi tunaanza mchakato huo mara moja kuanzia leo, wanaoajiriwa ni kuanzia ngazi ya cheti hadi Shahada kulingana na kada anayoiomba mhusika, kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 wasiozidi umri wa miaka 45.”

Hata hivyo ametoa angalizo kwa waombaji kuacha udanganyifu wa sifa za maombi yao na hata kwa wale wenye ulemavu ambao wametengewa nafasi kuwa watachukuliwa hatua na mamlaka za Serikali.

Amesema, waombaji wote wataomba kupitia mtandao wa Tamisemi na waliokuwa wameomba siku nyingi wametakiwa kuhuisha taarifa zao, na kutoa angalizo kuwa kwa waombaji watakaotuma maombi kwa njia ya barua au posta maombi yao hayatapokelewa.

Rais Mwinyi awagusa wenye mahitaji maalum kwa sadaka
Kalidou Koulibaly: Lampard anatosha Chelsea