Serikali ya Guinea-Bissau, imeagiza kusimamishwa kwa mishahara ya Walimu ili kuondoa madai ya udanganyifu kwenye orodha ya mishahara kutoka kwa wafanyikazi gushi.
Taifa hilo la afrika Maghaŕibi, ambalo linategemea kwa kiasi kikubwa misaada ya nje kukidhi mishahara katika sekta ya elimu, limetangaza vita dhidi ya watumishi wa Umma hewa ili kupunguza sehemu kubwa ya fedha, zinazoelekezwa kwenye mishahara.
Uamuzi wa Julai 18 wa Baraza la Mawaziri wa nchi hiyo siku ya Alhamis uliagiza wizara ya elimu kufanya sensa ya idadi ya wafanyikazi wake.
Rais wa Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embaló. Picha ya Ludovic Marin.
Hatuo hiyo itawathiri walimu 8,000 katika Shule za Msingi na Sekondari nchini humo ambao wanapata wastani wa faranga za CFA 50,000 ($86) kwa mwezi huku Rais wa muungano wa kitaifa wa Walimu wa Bissau, Domingos de Carvalho, akisema chama hicho kitakata rufaa dhidi ya uamuzi huo usio wa haki.
Nchi hiyo, ina idadi ya watu milioni 2.1 na asilimia 56 ya raia wake wana uwezo wa kusoma na kuandika huku de Carvalho akisema hawatapanga hatua yoyote ya mgomo, lakini wanafikiria kutafuta njia zingine kutafuta muwafaka.