Serikali kupitia Wizara ya Madini, imetangaza mnada wa madini aina ya Tanzanite utakaofanyika kuanzia tarehe 18 na kumalizika Desemba 28 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Madini, imesema kuwa mnada huo wa Tatu wa Kimataifa kwa Madini ya Tanzanite ghafi na yaliyokatwa, utafanyika Mererani Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

Aidha, mnada huo, utahusisha madini ya Tanzanite ghafi na yaliyokatwa kutoka Kampuni ya TanzaniteOne yenye ubia na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na madini kutoka kampuni ya Tanzanite Africa.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeongeza kuwa Kampuni mbalimbali za ndani ya nchi pia zinatarajiwa kupeleka madini ya Tanzanite kwa ajili ya kuuzwa kwa wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

Bashe: Sisi tulijaribu tukashindwa UVCCM
Muhimbili yatoa somo kwa watumishi wapya