Serikali imetangaza nafasi 6800 kwa Wanagenzi Vyuo vya Kati, watakaojiunza fani mbalimbali katika mwaka mpya wa masomo, unaotarajia kuanza rasmi Septemba 2023, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya zile za mwaka wa masomo uluopita.
Hayo yamebainishwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako wakati akiongea na wanagenzi kwenye chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya – MUST.
Amesema, mwaka wa masomo uliopita zilitangazwa nafasi 3765 kwa kuzingatia uhitaji mkubwa na dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwawezesha kupata ujuzi wa kuajiriwa au kujiari na kujikomboa kiuchumi.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka Vijana Wanagenzi kuwa wazalendo na mabalozi wazuri wa kuzitangaza kazi zinazofanywa na Serikali .