Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, ametangaza nafasi za ajira kwa walimu 6,949 wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na ajira 2,726 kwa kada mbalimbali za Afya.

Amesema ajira hizo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuajiri wafanyakazi zaidi ya elfu sita.

Akizungumza Jijini Dodoma leo Mhe.Ummy amesema ajira hizo zinakwenda kuziba mapengo ya wafanyakazi waliostaafu, waliofariki na wengine kuacha kazi hivyo ajira hizo ni za watanzania na kwa wale watakaokidhi vigezo watapatiwa ajira kwa haraka ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa ajira zitatolewa kwa haki na waombaji wasitoe fedha yeyote ili kupata ajira kwakuwa baadhi ya watu wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo.

Watu wenye sifa wanatakiwa kuomba kuanzia leo Mei 9 hadi 23, 2021.

PICHA: Rais Samia ashiriki Ibada ya kuaga mwili wa Teddy Mapunda
PICHA: Waziri Mkuu ashiriki Ibada ya kusimikwa kwa Askofu KKKT - Lushoto Tanga