Serikali imezuia shule binafsi kumrudisha darasa, kumfukuza mwanafunzi aliyefaulu mtihani darasa la 4, kidato cha 2 kwa kutofikia ufaulu wa wastani wa shule husika.

Waraka wa Elimu Namba 7 wa Mwaka 2004 umepiga marufuku utaratibu wa shule binafsi zisizomilikiwa na serikali kukaririsha Darasa, kufukuza au kuhamisha mwanafunzi aliyefaulu Mtihani wa Darasa la Nne, Kidato cha pili kwa kigezo cha wanafunzi hao kutofikia wastani wa ufaulu wa shule husika.

Shule itayokiuka agizo hilo serikali itachukuliwa hatua stahiki.

Hata hivyo wazazi na walezi waombwa kurudisha watoto wao shule waliofukuzwa kwa madai ya kutofikia wastani wa shule ili halali wamefaulu kulingana na alama za serikali.

Shule zimepewa siku kadhaa kurekebisha hilo kuanzia leo, 12 januari, 2018 mpaka kufikia 20 januari, 2018 watoto wote imeariwa wawe wamesharudishwa shuleni kwao ili kuendelea na masomo.

[​IMG]

Sababu ya Ronaldo kushika namba 49 duniani
Makonda afunguka kuhusu JPM