Jijini Dodoma, Bunge la 11 kikao cha 12 mkutano wa 11 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali imesema haioni haja ya kubadilisha sheria ya uzazi kwa sababu inampa fursa mwanamke kupumzika kutozaa mara kwa mara na kufuata uzazi wa mpango.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Utamishi na Utawala Bora, George Mkuchika wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Viti maalamu, Sonia Juma aliyetaka kufahamu mpango wa serikali juu ya kuwasaidia kina mama ambao wanajifungua kabla ya kipindi cha kuruhusiwa kupata miezi mitatu ya mapumziko ili waweze kuwanyonyesha watoto wao.

“Kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2009. Mtumishi wa umma anapojifungua hupewa likizo ya malipo ya siku 84 na iwapo atajifungua zaidi ya mtoto mmoja (mapacha) ataongezewa siku 14 na kuwa jumla ya 98. Endapo mtumishi atajifungua mtoto tena kabla ya kutimiza miaka mitatu atapewa likizo maalum ya wiki sita ili kuhudumia mtoto wake kwa mujibu wa kanuni na baada ya hapo serikali inaweza kumuongezea siku za kupumzika kulingana na ushauri wa daktari”, amesema Mkuchika.

Sonia alitoa hoja hiyo kufuatia sheria inayosema likizo ya uzazi kutolewa mara moja kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kuzingatia sera ya afya ya mama na mtoto.

Aidha amesisitiza kwa mashirika binafsi endapo mtu yeyote atanyimwa haki ya likizo ya uzazi, wizara itaarifiwr mapema ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mwajiri wake.

 

Video: Beyonce avunja rekodi mbili kwa mkupuo
Khaligraph Jones afunguka mpango wa kufanya kazi na Jay Z