Serikali imetoa Mwezi Mmoja kwa watu,Makampuni na Mashirika wanao durufu nakara zake kuacha mara moja tabia hiyo,na kwamba mtu yeyote atakaebainika baada ya muda huo kumalizika atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja kulipa faini kubwa na kufilisiwa mali zake zote atakazokuwa anamiliki.

Hayo yamesemwa na mchapishji mkuu wa serikali bw,Cassim .k.Chibogoyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake jijini Dar es salaam,bw, Chibogoyo aliongeza kuwa watu wamekua wakijiamria tu kufoji nyaraka za serikali bila kufuata utaratibu na kusababishia nchi matatizo makubwa.

Aidha aliagiza taasisi zote za serikali kupandisha na kushusha bendera zote za serikali kwa muda muafaka na kubadilisha bendera zote chakavu na kwamba popote pale penye bendera ya taifa lazima kuwe na bendera ya Afrika masharika.

Hata hivyo bw, Chibogoyo alitoa maelekezo ya matumizi mbalimbali ya nembo, wimbo  na bendera ya taifa  kuwa bendera na wimbo vitatumika katika shughuli za  sherehe za  kitaifa  kukiwepo na viongozi na kuondolewa pindi sherehe hizo zinapomalizika.

Pia alilisisitiza kuwa wimbo wa taifa ni dua pekee la nchi linalomtaja mungu na kuamini katika mungu hivyo kutahadharisha kuwa wimbo huo hauimbwi sehemu zingine zaidi ya shughuli za kitaifa na za kimataifa na mashuleni ili kutoa wigo mpana kwa wananchi kuufahamu.

Ofisi hiyo ilitoa wito kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuri  za kufanya kazi kwa bidii na kuiunganisha nchi kwa ujumla na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Video Mpya: Kala Jeremiah Ft Miriam Chirwa – Wanandoto
Makonda anasa ufisadi mkubwa ujenzi wa jengo la Machinga complex