Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Fortunatus Musilimu, amesema kuwa atawachukulia hatua kali wavunjifu wote wa sheria za usalama barabarani pasipo kujali nyadhifa, madaraka na umaarufu wa mtu husika katika jamii

Onyo hilo limetolewa Jijini Dar es salaam na ACP Musilimu wakati akitoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshiriki shindano la uelewa wa sheria za barabarani kupitia michoro mbali mbali

Aidha,  shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya mafuta ya Puma Energy ambaYo serikali inaumilikia wa asilimia hamsini, kwa lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa shule mbalimbali.

Hata hivyo, kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti amesema shindano hilo pamoja na programu nyingine za usalama barabarani zinazofadhiliwa na kampuni hiyo zinalenga kujenga kizazi kitakachokuwa na uelewa wa juu kuhusu usalama barabarani ili kulinda nguvu kazi ya taifa inayohitajika katika uzalishaji.

Trump azionya Iran, Korea Kaskazini na Venezuela
Kikongwe kuishi karibu na Ikulu, Mkuu wa Mkoa aagiza