Wakati mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukitarajiwa kuanza hivi karibuni, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewaonya wafanyabiashara watakaopandisha bei za vyakula hususani vinavyotumika kwenye mfungo huo.

Amesema hayo leo Aprill 11, 2021 ofisini kwake Unguja wakati akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban amesema watakaopandisha bei hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Mimi binafsi nitazunguka katika maeneo mbalimbali ya biashara kujiridhisha kama kweli wafanyabishara wanafuata maeekezo ya serikali na ijulikane kwamba zipo adhabu kali watakaokiuka taratibu,” amesema waziri

Licha ya Sheria ya Ushindani na Kumlinda Mlaji namba tano ya mwaka 2018 kutobainisha adhabu kamili anazotakiwa kuchukuliwa anayekwenda kinyume, waziri amesema faini hiyo watakayotozwa inaweza isiwe chini ya Sh milioni moja.

“Kumekuwapo na tabia ya muda mrefu ya baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa kutumia fursa ya mwezi mtukufu kupandisha bei kiholela hasa kwa bidhaa muhimu kama mchele, sukari na ngano.

“Tabia kama hizi kutaka kuchuma faida kupitia mgongo wa wanaofunga hazikubaliki na mara nyingi husababisha wananchi wenye wa maisha duni kutekeleza ibada yao ya funga katika mazingira magumu,” amesema

Mbowe amkumbuka JPM, "Alifanya kazi usiku na mchana"
Juisi ya karoti kinga dhidi ya Saratani