Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina malengo makubwa juu ya elimu inayotolewa nchini na kama ilivyoanza kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekendari kidato cha 1 hadi cha 4, imesema huko mbeleni itatoa elimu bure hadi chuo kikuu.
”Naomba nimuhakikishie Mh. Mbunge ni kwamba lengo la serikali huko mbele kadiri uwezo utakavyo ruhusu tutatoa elimu ikiwezekana hadi chuo kikuu bure,” amesema Nasha.
Nasha ameyabainisha hayo, leo Juni 14, 2018 Bungeni Jijini Dodoma katika kikao cha 11 mkutano wa 51 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje aliyehoji mpango wa serikali katika kutoa elimu bure kwa darasa la 13 na 14 yaani kidato cha 5 na 6.
-
VideO: ‘Sinema’ ya Lembeli akirudi CCM, Vigogo 6 Bodi ya Mikopo Kitanzini
-
Video: Nilihisi kama nimeokota ‘dodo’- Mzee Mashaushi
“Kwa kuwa elimu bure ni kuanzia la kwanza mpaka la kumi 12 lakini kidato cha tano na cha sita hawamo, hawa wote ni watoto wa mtu mmoja kuna sababu gani za msingi form five na Six wakaacha kusamehewa karo kwahiyo? ninaomba Waziri atoe maelezo wote watoto ni wa kwake kwanini hao waachwe?. amesema Lubeleja.
Nasha amesema kwa sasa mchakato huo sio rahisi kufanyika kutokana na uchache wa rasilimali fedha, hivyo amesisitiza kuendeleza utaratibu wa utoaji elimu bure kwa shule za ngazi za awali yaani shule za msingi hadi kidato cha nne hadi hapo serikali itakapokuwa vizuri kifedha na kuhudumia elimu bura kuanzia awali hadi chuo kikuu.
”Uwezo ukiongezeka hatuna shida ya kuongeza kidato cha tano na cha sita, lakini vilevile kama mnavyofahamu serikali inatoa mikopo kwaajili ya wanafunzi wa elimu ya juu kwahiyo anachosema ni kitu cha kweli kwahiyo uwezo ukiongezeka kidato cha tano na sita elimu bure.” Nasha.