Serikali imewahakikishia wananchi wa vijijini kupata umeme wa uhakika kupitia miradi yake ya REA ya awamu ya tatu kwa bei nafuu ili waweze kuongeza vipato vyao kwa vile gharama zote zitabebwa na Serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kibaha vijijini wakati wa uzinduzi wa mradi wa REA awamu ya tatu ya kusambaza umeme vijijini kwa Mkoa wa Pwani uliofanyika Mlandizi.

Amesema kuwa pamoja na Pwani kupewa kipaumbele katika huduma ya umeme mkubwa kwa vile viwanda vingi vitajengwa huko, pia mikoa mingine itapata umeme kulingana na mpangilio wa Serikali.

Kwa upande wao wananchi wa Jimbo la Chalinze na Kibaha Vijijini wamezungumzia changamoto zinazowakabili kwenye mahitaji mapya  ya umeme.

Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesema mradi wa REA namba tatu utamaliza kiu ya wananchi wa Pwani kupata huduma hiyo huku akielezea kero ya wananchi katika kuunganishiwa umeme na Tanesco ikiwemo upatikanaji wa Nguzo.

Watumishi wa umma watakiwa kuchangamkia fursa
Mtu mmoja apigwa risasi na kufa mkoani Singida