Serikali imetoa onyo kwa watu wanaoiadhibu mifugo hususan katika maeneo yenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mkurugenzi wa Huduma za mifugo nchini katika wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Abdu Hayghaimo aliwataka watu wanaoiadhibu mifugo katika migogoro hiyo kuacha mara moja kwani mifugo hiyo huongozwa na binadamu katika maeneo yasiyohusu wanyama.

Dk. Hayghaimo alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, wanyama wana haki ya kupata chakula, maji, matibabu na mahali pazuri pa kupumzika pamoja na kulindwa dhidi ya maumivu yoyote na mateso yanayoweza kusababishia kifo.

Aliwatahadharisha wakulima na wafugaji kutochukua sheria mikononi na kuwadhuru wanyama katika migogoro kati yao kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na haki za wanyama.

Profesa Maghembe amwagia Sifa Nyalandu, Aahidi kuendeleza Aliyoyaacha
Lukuvi aagiza watumishi kufanya kazi hadi Usiku, Abaini Urasimu Mkubwa Wizarani