Serikali nchini, imeongeza miezi mitatu ya notisi hadi Desemba 31, 2023 kwa baadhi ya wafanyabiashara na wakazi waliopanga katika nyumba za shirika la nyumba la Taifa – NHC, eneo la Kariakoo.

Uamuzi huo, umetangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula wakati wa mkutano wa pamoja wa wizara hiyo, NHC na uongozi wa wapangaji.

Alisema, “Kariakoo ni miongoni mwa maeneo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho na tunatarijia kuwa baada ya maboresho hayo haitakuwa Kariakoo kama ya sasa, itakuwa nyingine.”

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia maombi ya wapangaji hao, kuiomba Serikali kuwaongezea muda na kuwapa kipaumbele, pindi uendelezaji wa maeneo waliyopo utakapo kamilika.

Rais awataka wakuu wa usalama kustaafu
Mwendokasi: LATRA yashusha rungu kwa Mabasi tisa