Serikali imekitaka Chama Cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) kuwasilisha malalamiko rasmi juu ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaovunja haki za wafanyakazi.

Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeani Sefue amesema kuwa watumishi wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwenye vyombo vya habari na badala yake watoe malalamiko hayo kwa njia rasmi.

Alitaja malalamiko hayo kuwa ni pamoja na wakuu wa wilaya kuwatia selo kwa muda wa saa 6 baadhi ya watumishi na wakuu wa mikoa kuwanyima likizo.

Hata hivyo, Balozi Sefue alisema kuwa hadi sasa bado hawajapata malalamiko yoyote ingawa wamekuwa wakisikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa wakuu wa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro wamefuta likizo kwa wafanyakazi wa serikali kwa madai ya kuwataka wafanye kazi tu.

Chris Brown Amzawadia Gari La Kifahari Mwanamke Aliyenyanyaswa
Gazeti Lililochapisha Habari Za ‘Kifo’ Cha Father Christmas Latoa Ufafanuzi