Mawaziri wakuu wastaafu waliohama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na vyama vya upinzani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye waliibuka katika mjadala wa Bunge jana baada ya mbunge kuhoji uhalali wao wa kuendelea kulipwa posho na stahiki nyingine.

Mbunge wa Dimani, Hafidh Ali Tahir aliitaka serikali kulitolea ufafanuzi suala la mawaziri hao wakuu kuendelea kulipwa huku akiwataka kama waroho wa madaraka, kwani nguvu ya uwaziri Mkuu waliipata wakati wakiwa CCM.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angela Kailuki aliliambia Bunge kuwa viongozi hao wastaafu wana haki ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote cha siasa hivyo hawakufanya kosa.

Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye walipokuwa CCM

Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye walipokuwa CCM

“Sheria inatamka kwamba mtu yeyote anayo haki ya kujihusisha na mambo ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kujiunga na chama chochote. Mawaziri Wakuu wastaafu, kama walivyo watu wengine wanao uhuru wa kujiunga na chama chochote cha kisiasa wanachopenda ili mradi hawavunji sheria,” alisema.

Alisema kuwa pendekezo la kutaka viongozi hao kufutiwa posho kwa sababu za kisiasa itakuwa ni kwenda kinyume na matakwa ya katiba ya nchi.

“Kwakuwa haki ya kujiunga na chama chochote au kujihusisha na masuala ya kisiasa ni ya kikatiba, na kwakuwa haki hizi haziwezi kuzuiwa au kuingiliwa, ni wazi kwamba suala la kufanyia marekebisho sheria ya mafao kwa viongozi wa kitaifa wastaafu, sheria namba 3 ya mwaka 1999 kwa lengo la kuwazuia mawaziri wakuu wastaafu au viongozi wengine wastaafu kujiunga na chama chochote cha kisiasa itakuwa ni kwenda kinyume na katiba ya nchi,” aliongeza.

Bashe ameungana na Ukawa? Zitto na Mbowe warejesha ‘kicheko’
JKU Kupiga Kambi Uganda Kwa Ajili Ya Gabarone United