Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji wa watanzania kwenda nje ya nchi kufanya kazi endapo itabaini kuwa wanawapeleka huko kuwauza miili yao na sio kuwaunganisha katika kazi rasmi kama walivyokubaliana.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba wakati akijibu la nyongeza la Mbunge, Hawa Mchafu aliyetaka kufahamu serikali imechukua hatua gani za kisheria dhidi ya wafanyabiashara hao.

“Kama taarifa hiyo itajulikana kuwa ni kweli, hatua za kisheria za nchi yetu zitachukuliwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo lakini mpaka sasa mimi sina taarifa za aina hiyo,” amesema Dkt. Kolimba.

Hata hivyo, Dkt. Kolimba amesema yeye pamoja na Wizara yake watafuatilia madai ya watanzania wanaosafirishwa kwenda na nje ya nchi na kuchukuliwa figo zao na kuuzwa ili waweze kuwachukulia hatua kali.

 

Nyota wa Chelsea watemwa kikosi cha taifa Spain
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike  Hispania