Serikali imesema kuwa utaratibu wa kuwahamisha vituo vya kazi watumishi wa umma waliofanya makosa haukubaliki katika awamu hii.

Akiongea katika ufunguzi wa semina elekezi kwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliwataka viongozi hao kulisimamia agizo hilo la serikali kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa nidhamu katika wizara husika.

Aidha, Balozi Sefue aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha za umma kwa kuwa serikali haitarajii kuwepo hati za ukaguzi wa hesabu zenye kasoro.

Watumishi kuadhibiwa

Makongoro Mahanga Amkosoa Magufuli
Zari: Tiffah Ni Rais Wenu ajaye