Serikali imeyaagiza makampuni ya Bima hapa nchini kuhakikisha yanaajiri watanzania badala ya sasa kuajiri wageni kutoka nje ya nchi ambapo ni makampuni matano tu hapa nchini yanaendesha bima ya maisha kati ya makampuni 31.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa ufungua mkutano wa Taasisi za bima kutoka nchi 20 za bara la Afrika (African Insuarence Organization).
Amesema kuwa serikali ya Tanzania kwa sasa imejikita kwenye uchumi wa viwanda na mchango wa sekta hiyo unahitajika kufikia malengo tarajiwa ya kukuza uchumi.
Aidha, ameagiza sekta hiyo kuangalia upya muundo wa bima ya maisha ilikuweza kuendana na sera za nchi hususani ya viwanda bila kusahau kilimo itakayosaidia watanzania wengi kukua kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi.
“Nimatarajio yangu kuwa sekta ya bima hapa nchini itasaidia ukuaji wa kiuchimi kwa wananchi kuweza kujiunga kwa wingi na hili natarajia kwa siku mbili mtakazokaa hapa mtajadili ni namna gani mtaweza kuisaidia serikali kuweza kukuza uchumi hususani wa viwanda kwa malengo mtakayojiwekea,”amesema Dkt Kijaji
Kwa upande wake Kamishna wa Bima nchini, Baghayo Saqware amewambia kuwa wananchi wengi wanahitajika kuanzisha uwakala wa bima ilikuwezesha kukuwa kwa sekta hiyo ambayo wageni ndio wenye makampuni mengi kuliko wazawa hivyo ni fursa adhimu kwani vigezo vya kuanzisha uwakala vinalingana na sifa za watanzania wengi wa chini.