Serikali ya Mkoa wa Tabora imetoa onyo kwa Kampuni zote za usambazaji pembejeo za zao la Pamba kuhakikisha mbegu na dawa za kuua wadudu watakazopeleka kwa wakulima ni bora na hazina matatizo ili zisije zikawasababishia hasara wakulima.

Onyo hilo limetolewa wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wa kuwaelimisha wakulima juu ya kulima zao hilo kwa kufuata Sheria na taratibu zake ili kuongeza ubora.

Amesema kuwa Kampuni hizo zilizopewa kazi ya kusambaza Mbegu kwa wakulima wa pamba katika Wilaya Tano za Mkoa huo ni vema zikapeleka mbegu bora na zilizopendekezwa kulima zao hilo ni vema zikahakikisha kuwa zinapeleka kwa wakulima mbegu iliyopendekezwa ya UKM08 ambayo iko katika ubora na wakawa na uhakika kuwa inatoa ili kuwaepusha wakulima kupoteza nguvu zao.

Aidha, amesema kuwa ni vyema wakahakikisha dawa watakazosambaza kwa wakulima wa Pamba katika maeneo ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuua wadudu zikawa ni zile zilizopendekezwa na zina uwezo kweli wa kuua wadudu haribifu na kuongeza kuwa kinyume cha hapa atawakamata wao na wali zao ili waweze kufidia hasara kwa mkulima.

“Najua nyie Kampuni zilizopewa jukumu la kusamabaza mbegu kwa wakulima na dawa mtapeleka mbegu bora na zilizokubalika, ikitokea kuwa mbegu mlisambaza kwa wakulima zikashindwa kuota na dawa ikashindwa kuua wadudu, mimi nitakachofanya ni kukamata mali zenu zote ili ziuzwe kufidia hasara ambayo wakulima watakuwa wamepata,“ amesema Mwanri

Kwa upande wa Meneja  kutoka Kampuni ya Quton Tanzania limited iliyozalisha Mbegu zinazosambazwa katika maeneo mbalimbali Phineas Chikaura alisema kuwa mbegu hiyo inasambazwa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya yaNzega inao ubora ambao umedhibitishwa na Taasisi ya utafiti wa Mbegu hapa nchini.

Serikali kudhibiti usafiri wa majini
Kishapu yapanga mikakati ya maendeleo