Serikali imesema kuwa haitasita kuzifuta na kuzinyang’anya leseni Kampuni ambazo zinanunua pamba hapa nchini ikiwa zitachelewesha fedha za wakulima wa zao hilo na kuanza kuwazungusha bila kuwalipa fedha zao.
Hayo yamesmwa na Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba wakati akizindua ununuzi wa Pamba katika Kijiji cha Muhilidede wilayani Uyui Mkoani Tabora
Amesema kuwa ni jukumu la Kampuni zinapomaliza kununua pamba ya mkulima ni kumlipa palepale siku hiyo hiyo kwa kuwawekea fedha katika Akaunti zao au kupitia simu ya mkononi na kisha pesa ikishaingia aone ujumbe wa kumhakikisha kulipwa.
Dkt. Tizeba amesema kuwa Serikali inachukua hatua hiyo ili kurejesha imani kwa wakulima juu ya ushirika ambao umekuwa ukipigwa vita na baadhi ya watu.
Aidha Waziri huyo amewaagiza Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kuhakikisha vinawakamata na kuwapeleka Polisi watu wote ambao watapeleka pamba iliyochanganywa na uchafu na ile iliyowekewa maji kwa sababu watu hao ni sawa na wezi.
-
Kesi ya Mbowe na wenzake yagonga mwamba, wataka rufaa
-
Serikali kuchakachua sheria ya Uzazi na Afya, wanaume nao watajwa kunufaika
-
UDSM yapata pigo, wanafunzi watatu wafariki dunia
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kutumia sehemu ya asilimia 33 ya kila kilo watakayopata kununua Matrekta ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo msimu ujao.