Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amewajulia hali majeruhi wa ajali ya basi la kampuni ya Ally’s Star lililogonga treni ya Mizigo katika makutano ya barabara na Reli mjini Manyoni, Mkoani Singida.

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ya ile Misheni ya St. Gasper iliyopo Itigi, takriban kilometa 38 kutoka eneo la ajali hiyo iliyotokea leo Novemba 29, 2023 majira ya saa 11, alfajiri.

Katika ajali ya Basi hilo lenye namba T178 DVB , watu 13 wamefariki ambao ni wanawake sita, wanaume saba na majeruhi 25, wanawake saba, wanaume 18 na liligonga kichwa cha treni chenye namba V951 9006 kilichokuwa kikitokea Stesheni ya Aghondi kuelekea Manyoni Mjini.

Hata hivyo, mapema hii leo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dkt. Furaha Mwakafira alisema walipokea miili ya watu 13 na majeruhi hao ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.

Wanaowatumikisha Watoto muda wa Masomo waonywa
CCM yawakingia kifua Wasafirishaji Dodoma