Kesi ya aliyekuwa mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi imeahirishwa hadi Agusti 17, 2017 ili kuruhusu mshtakiwa huyo kupata matibabu ya kiafya.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ leo August 3, 2017 imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Harbinder Singh Sethi hatotibiwa nje ya nchi wala Hospitali ya Muhimbili, bali atatibiwa Hospitali ya Amana na Lugalo.
Matibabu hayo yatafanyika Hospitali ya Lugalo na Amana na sio nje ya nchi kama ambavyo ilidhaniwa kutokana na sababu za kiusalama na kuwa Sethi hakuwa na vigezo vya kutibiwa nje ya nchi wala Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
-
Utafiti: Raila apata ushindi mwembamba dhidi ya Uhuru
-
UN yatoa ripoti ya hali ya kisiasa nchini Burundi
-
Maalim Seif amwaga ugali baada ya Lipumba kumwaga mboga, amtimua Sakaya
Aidha, Swai amedai watampeleka Sethi Hospitali ndani ya siku 14, ameyaeleza hayo baada ya Wakili wa utetezi, Alex Balomi kudai kwamba hadi sasa Sethi hajapewa matibabu licha ya Mahakama kuamuru atibiwe.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu shahidi amesema hakutoa amri ya Sethi kutibiwa nje ya nchi, bali alitoa amri ya kutibiwa ikiwezekana Muhimbili, hivyo ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha ndani ya siku 14 mshtakiwa anapatiwa matibabu.