Mabingwa wa Europa League Sevilla CF wamekamilisha dili la kumnyakua beki wa kushoto kutoka nchini Argentina Marcos Javier Acuña, akitokea klabu ya Sporting CP ya Ureno.

Sevilla CF inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), imemsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa ajili yakuziba nafasi ilyoachwa wazi na Sergio Reguilon alierejea Real Madrid.

Reguilon alijiungana Sevilla CF kwa mkopo msimu uliyopita na kufanikiwa kutwaa taji la Europa League, hali ambayo iliwatamanisha viongozi wa klabu hiyo kutaka kumsajili moja kwa moja, lakini Real Madrid waligomea dili hilo.

Acuña, amejiunga na Sevilla CF kwa ada ya Eyro Milioni 10 na jana Jumatatu alikamilisha utaratibu wa kupimwa afya.

Acuña, alitumia misimu mitatu na miamba ya ya Ureno, Sporting CP na kucheza mechi 134 katika mshindano yote.

Beki huyo ambaye amewahi kuitumikia timu ya taifa ya Argentina katika michezo 27 na kufunga mabao mawili, anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa Sevilla CF katika kipindi hiki, akitangiliwa na Ivan Rakitic kutoka FC Barcelona, Oscar Rodriguez kutoka Real Madrid, Yassine Bounou kutoka Girona na Jesús Joaquín Fernández Sáenz de la Torre *Suso*.

Sevilla ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga msimu wa 2019-20, na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA Champions League), huku ikitwaa ubingwa wa Europa League.

Kwa hatua huyo Sevilla CF itacheza mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa michuano ya Ulaya (UEFA Super Cup) dhidi ya mabingwa wa soka barani humo FC Bayern Munich Septemba 24.

IGP atoa maagizo ajali ya moto Kagera
Kocha Sven aanika mipango ya kuongoza Ligi Kuu