Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast, Seydou Doumbia amerejea nchini Urusi kujiunga na klabu ya CSKA Moscow kwa mkopo akitokea nchini Italia kwenye klabu yake ya AS Roma.

Doumbia, ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora mara mbili katika ligi ya nchini Urusi akiwa na klabu ya CSKA Moscow, anatarajiwa kurejea tena kwenye klabu ya AS Roma mwezi januari.

Mshambuliaji huyo anaondoka nchini Italia huku akikumbuka msoto wa kushindwa kufanya vyema kwenye ligi ya Serie A, baada ya kufunga mabao mawili kwenye michezo 13 aliyocheza.

Kurejea kwake nchini Urusi, kunaendelea kukumbusha mazuri yake kwa mashabiki wa klabu ya CSKA Moscow, ambapo amekubali kuvaa jezi namba 88 ambayo aliwahi kuitumia kabla ya kuhamia nchini Italia.

Seydou, tayari anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha CSKA Moscow, ambacho kitacheza mchezo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon juma lijalo.

CCM Wakamata Kadi Bandia, Wawatupia Lawama Wapinzani
Hamfrey Polepole, Mchungaji Msigwa Wakabana Kuhusu Lowassa Na Ukawa