Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.

Tukio la shabiki huyo kuingia uwanjani lilitokea jana Jumanne usiku muda mfupi baada ya PSG kufunga bao la tatu katika mchezo wa kalbu bingwa ambao wenyeji Celtic waliambulia kipigo cha mabao 5-0 katika uwanaja wao wa nyumbani.

Wakati huohuo klabu ya Paris St-Germain pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo wa Celtic Park.

Uefa inatarajia kutoa tamko rasmi juu hadhabu gani itatolewa baada ya kitengo chake maalumu cha nidhamu na maadili kushughulikia jambo hilo tarehe 19 mwezi Oktoba.

Kocha wa Celtic Brendan Rodgers alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.

”’Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri, inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya”, alisema Brendan Rodgers.

 

Kaskazini Pemba yaanza kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Shein
WCB waja na hizi mbili ''Nishachoka na Unaibiwa''