Wanawake watano waliovalia mabaibui na waliokua wamevaa mikanda ya kujilipua wamevamia kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.

Maaskali polisi mjini Mombasa wamesema kuwa wamelitibua jaribio hilo na kufanikiwa kuwauwa wanawake watatu huku wawili wakikamatwa na polisi.

Polisi wamesema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kutoa taarifa kuhusu simu ya mkononi ilioibiwa.

Wakati wakitoa maelezo yao yalipokuwa yakichukuliwa mmoja wao alichukua kisu na kuwachoma polisi wawili wa ,huku mwingine akiwarushia polisi waliokuwa wakichukua maelezo hayo bomu la petroli.Polisi waliwafyatulia risasi na kuwaua.

Polis waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.

Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika eneo la pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni mengi yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab

Marekani Yajipanga Kuishambulia Korea ya Kaskazini
Mapambano Kati ya Waasi Na Serikali Yazidi Kupamba Moto Nchini Syria