Shambulio la watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi huko Gaskindé, kaskazini mwa Burkina Faso limesababisha vifo vya askari watu 11 na raia 50 hawajulikani walipo.
Burkina Faso, ambako maafisa wa kijeshi walichukua mamlaka mwezi Januari wakiahidi kupambana na vita dhidi ya jihadi, inakabiliwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha yenye mafungamano wa al-Qaeda na kundi la Islamic State.
Tarifa ya jeshi imesema, “Msafara wa kusambaza idadi ya watu, ukisindikizwa na kitengo cha 14 cha RIA (Kikosi cha Silaha) kuelekea Djibo, ulikuwa lengo la shambulio la kigaidi karibu na eneo la Gaskindé, Sahel lililo katika Mkoa wa Soum.”
Septemba 24, 2022, msafara mwingine uliosindikizwa na jeshi, ambao uliondoka siku moja kabla kutoka mji mkuu wa eneo la Sahel, Dori hadi mji wa Sebba, ulishambuliwa na na wapiganaji wa IED ambapo watu wanne walijeruhiwa.
Siku ya Jumamosi, (Septemba 23, 2022), wanajeshi wawili na wasaidizi wawili wa jeshi la kiraia waliuawa katika shambulio la “kigaidi” kwenye doria katika jimbo la Tapoa, eneo lililopo mashariki mwa Burkina Faso likipakana na Niger na Benin.
Tangu mwaka 2015, mashambulizi ya mara kwa mara yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwakosesha makazi takriban watu milioni mbili.