Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio la kujitoa mhanga ndani ya msikiti mmoja uliofurika waumini kwenye mji wa Peshawar, ulilopo kaskazini magharibi mwa Pakistan imefikia watu 70.
Taarifa kutoka kwa Maafisa wa Serikali wa nchi hiyo, zinasema watu wengine 150 wamejeruhiwa kutokana na tukio hilo, na kuna wasiwasi idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Wengi ya waliouwawa ni Maafisa wa Polisi na inaarifiwa pia kulikuwa na takribani waumini 350 wakati mshambuliaji huyo alipojilipua.
Kamanda wa kundi la Taliban nchini Pakistan, amedai kuhusikana na shambulizi hilo ambalo limelaaniwa vikali na viongozi wa Serikali na upinzani, nchini Pakistan.