Takriban wanajeshi 17, na raia wanne wameuawa baada ya shambulio lililohusishwa na wanajihadi katika mji wa Tessit uliopo ukanda wa mpaka wa tatu kati ya Mali, Burkina Faso na Niger.
Jeshi la Mali, limethibitisha tukio hilo katika taarifa yake na kusema kuwa wanajeshi tisa pia wametoweka huku magari na vifaa vikiharibiwa.
“Bado ni wa muda na una uwezekano wa kubadilika, kulingana na taarifa hiyo ambayo ilisema imewaua maadui saba inawezekana kutoka kwa Dola ya Kiislamu katika Jangwa la Sahara na kunufaika na msaada wa ndege zisizo na rubani na mizinga kwa matumizi ya vilipuzi na mabomu ya gari.” imesema sehemu ya Taarifa hiyo.
Baadhi ya raia waliouawa walikuwa viongozi wa eneo hilo waliochaguliwa, jamaa za wahasiriwa waliambia waandishi wa Habari kwa sharti la kutotajwa majina kuwa maadui, pamoja na watu wengine saba waliuawa na kwamba jeshi linataja “idadi isiyojulikana ya waliokufa na waliojeruhiwa waliochukuliwa na washambuliaji.