Mamlaka za Serikali za nchi ni Somalia, zimesema idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya kundi la Kiislamu la Al-Shabaab katikati mwa nchi hiyo, imeongezeka na kufikia takriban watu 30.
Katika mashambulio hayo matatu tofauti, watu wengine 58 walijeruhiwa wakati magari matatu yaliyokuwa yamepakia vilipuzi yalipolipuliwa mjini Beledweyne, ulio katikati ya mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya wanamgambo wenye mafungamano na Al-Qaeda ambao wanadhibiti maeneo mengi ya Somalia.
Mamlaka hiyo imesema, “Tumethibitisha kwamba watu thelathini walikufa katika shambulio la hivi majuzi,” alisema Ali Jeyte Osman, gavana wa eneo la Hiraan ambako Beledweyne ndio mji mkuu.”
Miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo ni Waziri wa afya wa jimbo pana la Hirshabelle, na naibu mkuu wa wilaya, kufuatia washambuliaji wa kujitoa mhanga kulenga ofisi za serikali za mitaa.
Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wamesema kumekuwepo na uharibifu mkubwa baada ya mashambulizi yaliyodaiwa na Al-Shabaab, ambayo imeendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali kwa miaka 15.
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amelaani shambulio hilo, linalokuja wakati vikosi vya kitaifa, vinavyoungwa mkono na wanamgambo wa ndani na washirika wa kimataifa, vikiendesha kampeni kali ya kukabiliana na uasi dhidi ya tawi tanzu la Al-Qaeda.