Utawala wa kijeshi nchini Niger, umesema wanajeshi wake 29 wameuwawa kwa shambulizi la kigaidi, karibu na mpaka wa Taifa hilo na nchi ya Mali.
Waziri wa Ulinzi wa Niger, Luteni Jenerali, Salifou Mody amesema zaidi ya wapiganai 100 wanaotumia mabomu ya kuundwa nyumbani, wamekuwa wakiwalenga walinzi wa usalama wa taifa hilo ambao wapo katika ulinzi wa mpakani.
Hili ni shambulio la pili lenye kuwalenga wanajeshi wa Niger kwa juma hili pekee na hata hivyo Mody alisema Magaidi hao walidhibitiwa na nyenzo zao za vita ziteketezwa yakiwemo magari 15 na baadhi ya silaha kutekwa.
Utawala wa kijeshi wa Niger, ambao umechukua madaraka baada ya mapinduzi ya Julai 2023 dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia, umetangaza siku tatu za maombolezo.