Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, Dar es Salaam leo Machi 31, 2021 imewahukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara Abdul Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41) baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na dawa za Kulevya aina ya Heroin .

Mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali za Serikali, huku dawa hizo zikitakiwa kuteketezwa.

Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa na Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba watuhumiwa wamekutwa na hatiani katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.

Wawili hao walishtakiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.

Kocha Burundi: Tanzania haikutuzidi sana
Mbunge wa viti maalum Chadema atoa angalizo mafunzo JKT