Muigizaji wa kike wa filamu za Kiswahili, Shamsa Ford amesema kuwa hayuko tayari kuihama timu ya Ukawa inayoundwa na vyama vinne vya upinzani, kwa sababu ya kupewa fedha na CCM.

Amesema yeye anahitaji mabadiliko kwa kuwa kilio cha wasanii kuibiwa na kazi zao kimeshindwa kuzaa matunda kwa muda mrefu licha ya kuwepo ahadi za kukifanyia kazi.

“Mimi nitabaki huku kwa kuwa nahitaji mabadiliko,kila siku wasanii tunalia tukidai tunaibiwa na hakuna utekelezaji na matokeo yake tunapewa ahadi zisizoisha.”Amesema Shamsa.

Hata hivyo, haijafahamika kama timu ya CCM iliwahi kutaka kumpa fedha ili ajiunge na kambi ya wasanii wanaoiunga mkono au la.

sHAMSA

Shamsa Ford amekuwa akionesha msimamo wake wa kupinga hasa kampeni zinazofanywa na CCM kwa kuizungumzia afya ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa ambaye yeye anamuunga mkono.

“Binadamu yoyote ambae ana hisia , hofu ya Mungu,na huruma hawezi kumcheka mwanadamu mwenzie ambae anaumwa au kusumbuliwa na chochote kwasababu kabla hujafa hujaumbika. .Mungu akiamua kuonesha miujiza yake ni ndani ya sekunde tu…TUWE NA HURUMA NA UPENDO kwa wenzetu” aliwahi kuandika kwenye Instagram.

Jaji Lubuva Aonya Wanasiasa Wanaotumia Maneno Haya
Marco Silva: Nitavunja Mwiko Wa Kufungwa England