Meneja wa klabu ya Man utd, Jose Mourinho, usiku wa jana alijikuta akiingia katika mzozo na wachezaji wa Man City baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Inaelezwa kuwa, baada ya mchezo huo ambao ulishuhudia Man City wakichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja, wachezaji wa Man City walishangilia kwa sauti ya juu pamoja na muziki katika vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani hapo, kitendo ambacho kilipoteza utulivu.

Baada ya kuona hivyo, Mourinho akaamua kuelekea kwenye vyumba hivyo akiwa na straika wake Romelu Lukaku, lakini baada ya kuwambia wapinzani wao hao watulie bado wakaendelea kupiga kelele huku kipa wa Man City Ederson, akiwa ndiyo kinara wao.

Imeelezwa kuwa wakati wa tukio hilo, Mourinho alirushiwa kopo tupu la maziwa japo kuwa baadaye Man City walikana kutokea kwa tukio hilo.

Kipa huyo wa Man City na Mourinho walitoleana maneno ya kufokeana kutokana na kilichotokea.

Kili Stars kukamilisha ratiba, kocha apania kuondoka na point
Wapinzani wapigwa marufuku kushiriki uchaguzi