Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uswiz, Xherdan Shaqiri amefanyiwa vipimo vya afya yake kwa mafanikio makubwa ikiwa ni sehemu ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Inter Milan kuelekea Stoke City huko nchini England.

Shaqiri, alifanyiwa vipimo hivyo jana jioni baada ya kuwasili nchini England mwishoni mwa juma lililopirta na kushuhudia mchezo wa ligi ambapo klabu anayotarajia kuitumikia Stoke City ilikua ikipambana na majogoo wa jiji Liverpool, ambao walibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Kukamilika kwa hatua ya vipimo vya afya ya winga huyo, kunatoa mwanya kwa viongozi wa klabu ya Stoke City, kufanya mazungumzo na Shaqiri ili kukubaliana maslahi binafsi kabla ya kusaini mkataba.

Klabu ya Inter Milan ambayo ipo chini ya ukufunzi wa meneja Roberto Mancini ilimsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi januari mwaka huu, akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.

Inter Milan wamefikia maamuzi ya kumuuza nchini England, Shaqiri baada ya kuona hapendezwi na maisha ya nchini Italia na aliwahi kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema hivyo.

Ada ya usajili ya Shaqiri imeshatajwa kuwa nia Euro million 17 ambazo ni sawa na paund million 12, na italipwa mara baada ya taratibu zote kukamilishwa huko Britannia Stadium.

Taifa Stars Yaanza Mazoezi
CCM Wakamata Kadi Bandia, Wawatupia Lawama Wapinzani