Nyota wa zamani wa Newcastle Utd Alan Shearer amesema anaamini wachezaji wa Arsenal wamekubaliana na maamuzi ya Meneja wao Mikel Arteta kuhusu kumvua unahodha Aubameyang pamoja na kumtoa kwenye mipango yake kwa sasa.
Aubameyang alikumbwa na kadhia hiyo mwanzoni mwa mwezi huu Desemba, kufuatia utovu wa nidhamu wa kuchelewa kambini.
Shearer amesema: “Ilikuwa uamuzi mkubwa na wa kijasiri kutoka kwa Arteta kufanya kile alichokifanya kwa sababu Aubameyang ni nahodha na mshahara ambao analipwa ni mkubwa,”
“Lakini lazima aonyeshe nidhamu kwa sababu ana timu ya vijana ambayo anajaribu kutuma ujumbe. Sasa wanajua kwamba hawawezi kufanya fujo wala kuchelewa mazoezini”
“Kwa hali hii inaonekana wachezaji wamekubaliana na uamuzi ambao Arteta alifanya kwa sababu wanaonekana tu kwa namna wanavyocheza”
“Arteta alihitaji wachezaji wake kumuunga mkono katika suala la kumpa kile anachokihitaji kiuchezaji, na wamefanya hivyo kwa mtindo mmoja.”
Chanzo: BBC