Sheikh Jassim mambo yake yanakwenda poa kwa kuwa anakaribia kufikia makubaliano ya kuwa mmiliki wa Manchester United baada ya mazungumzo ya mwisho kupiga hatua.
Ilikuwa Novemba 22, mwaka jana wakati familia yenye utata ya Glazer ilipotangaza kwa mara ya kwanza nia yao ya kuiuza klabu hiyo, jambo ambalo lilipongezwa na mashabiki wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiwatusi Wamarekani hao.
Sheikh Jassim na chifu wa Ineos, Sir Jim Ratcliffe waliibuka kuwa mstari wa mbele na zabuni ya mfanyabiashara huyo wa Uingereza ikiwa ni pamoja na tahadhari ambayo inawaweka Avram na Joel Glazer kama washikadau.
Hata hivyo, ofa yake ya jumla haifikii.bei ya Pauni Bilioni 6 ambayo mpinzani wake sasa ameandaliwa na amekubali kuitoa.
Gazeti la The Sun limeripoti kwamba mazungumzo ya hivi karibuni yamekuwa yakiendelea, huku Sheikh Jassim akikaribia kuchukua nafasi hiyo.
Jassim raia huyo wa Qatar sasa anasemekana kwa sasa anakamilisha baadhi ya vitu kabla ya kufanikisha ununuzi, ingawa inaweza kuwa mwishoni mwa Novemba wakati taratibu zote zitakapofanywa.
Familia ya Glazer waliichukua United mwaka 2005 na muongo wao wa kwanza kwenye usukani ulidhihirishwa na wingi wa mataji makubwa, likiwemo taji la tatu la Europa.