Katika kudhihirisha kuwa dini ni mfumo wa maisha na tofauti za kiimani hazitofautishi utu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salim amehudhuria ibada katika kanisa la Ufufuo linaloongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’.

Sheikh Salim aliwaambia waaumini wa kanisa hilo kuwa anafurahi kuona Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani bila kujali tofauti iliyopo ya imani ya dini.

Sheik Mkuu Dar 2

Aidha, amewapongeza waumini wa kanisa hilo na viongozi wao kwa jinsi wanavyoshiriki katika shughuli za kijamii za maendeleo kama huduma za afya na elimu.

Sheikh Salim ambaye ni mjumbe wa Kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam, aliwasihi waumini hao kuendeleza undugu wao na waumini wa dini ya kiislamu ili kuendelea kujenga umoja wa Kitaifa.

Mwezi uliopita, Rais John Magufuli alimtembelea Mzee wa Upako na kuahidi kutengeneza barabara lililokuwa linapita karibu ya kanisa hilo.

Mambo 5 ya maajabu ya ‘tendo la ndoa’ unayopaswa kuyafahamu 18+
Video: Wanasoka na mbwembwe za kupotezea muda uwanjani