Mwanariadha kutoka nchini Jamaica, Shelly-Ann Fraser-Pryce amewakalisha wapinzani wake katika mbio za mita 100 upande wa wanawake huko mjini Beijing nchini China yanapofanyika mashindano ya dunia ya riadha.

Sherry alionekana kukabiliana kwa ukaribu na mwanariadha kutoka nchini Uholanzi Dafne Schippers lakini alifanikiwa kumshinda kwa kutumia muda wa sekunde 10.76.

Ushindi huyo unamfanya Sherry kufikisha medali za dhahabu sita, baada ya kufanya maajabu kama hayo katika michuano ya 100 na 200 mwaka 2013.

Schippers ambaye ni bingwa wa michuano ya Heptathlon alijinyakulia medali ya fedha na kuweka rekodi katika taifa leke.

Schippers mwenye umri wa miaka 23, alianza kushiriki michuano ya mbio fupi mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Katika hatua nyingine mwanariadha wa Nigeria, Blessing Ogakbare aliyepigiwa upatu kufanya vizuri katika mbio za mita 100 alimaliza wa mwisho.

Mwadui FC Kujipima Kwa Mabingwa Wa Kagame CUP
Wakenya Wafanya Kweli Mjini Beijing