Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9, 2020 zitumike katika kununulia vifaa mbalimbali kwa ajili ya Hospitali ya Uhuru.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Magufuli ameagiza fedha hizo zilizokuwa zimetengwa kiasi cha Sh. Milioni 835,498,700 sasa zitatumika kununulia vifaa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya Uhuru ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92na inatarajiwa kufunguliwa Desemba 30 mwaka huu.

Rais Magufuli ameagiza siku hiyo itumike kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii nchini. 

Kauli mbiu ya maazimisho ya 59 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka huu inasema ‘Miaka 59 ya Uhuru na Miaka 58 ya Jamhuri: Tanzania yenye Uchumi Imara Itajengwa na Watanzania Wenyewe, Tufanye Kazi kwa Bidii, Uwajibikaji na Uadilifu.’

Rapa Casanova mikononi mwa FBI
Koeman aukubali muziki wa Barcelona

Comments

comments