Licha ya vyombo vya habari kuonekana kuwa huru wadau wa sekta habari wanaamini kuwa utapatika kwa uhakika sheria ya huduma za vyombo vya habari ikifanyiwa marekebisho.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati wa kongamano la maendeleo ya sekta ya habari ambalo limefanyika Jiji Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau takribani 1000.
Balile amesema kuwa Serikali ya Rais Samia imesaidia kulegeza ugumu uliokuwa unaikabili sekta hiyo na kuvifanya vyombo vya habari hapa nchi kutokuwa na uhuru.
Kua wakati sheria kwenye sekta ya habari zilikuwa kitanzi magazeti yalifungiwa na uhuru ukapotea kabisa, ilivyokuja serikali ya awamu ya sita yamefanyika maboresho makubwa” amesema Balile
”Hata hivyo tunaamini utulivu tulionao utalindwa kisheria baada ya kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya huduma za habari kama ambavyo tumeahidiwa” amesema Balile