Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza kuangalia upya kwa sheria ya PF3 ambayo inamtaka muhanga wa ajali kupata kibali maalum kutoka kituo cha Polisi ili aweze kupata huduma ya kwanza ambapo amesema kuwa Sheria hiyo inasababisha watu kupoteza maisha katika mchakato wa kupata kibali hicho.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 katika uzinduzi wa kiwanda cha ushonaji katika bohari kuu ya jeshi la polisi nchini kilichopo eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.

Aidha Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kutotumia sheria na makosa ya barabarani kama kitega uchumi badala yake wajielekeze katika kutoa elimu ya barabarani.

“Jeshi la Polisi sheria zetu tunazozitunga ni sheria za udhibiti sasa tusijielekeze sana kutumia sheria na ile copomnent ya makosa na adhabu kwamba ni kitega uchumi”, Amesema Rais Samia.

Katika hotuba yake ametaja miongoni mwa vigezo atakavyotumia katika kuteua na kutengua makamanda wa mikoa ikiwemo udhibiti wa vitendo vya ujambazi.

”Najua IGP umeniletea majina ya kadhaa ya makamishina wawili wa fedha na lojistiki lakini hiki kitakuwa moja ya kigezo nitakachotumia”. amesema Rais Samia.

India: Maambukizi Covid-19 yapindukia Mil. 25
Serikali yajipanga kukabiliana na ujambazi mitandaoni