Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kwa kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta mambo yake.
Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48, sasa Infantino akimtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza baadhi ya sheria nyingi mpya katika soka. Baadhi ya sheria hizo ni kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka yaani offside.
Aidha Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati na kutaka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane. Kupunguza adhabu mipira ya kushika.
Van Basten anataka kadi iwe ya njano. Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi. Kupunguza idadi ya mechi kutoka 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu. Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA, na sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.