Mgombea urais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania, kupitia Chama cha ADA TADEA, John Shibuda, amesema kuwa utawala wa majimbo utawagawa wananchi.
Mgombea huyo aliyewahi kuwa mwanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) miongo miwili iliyopita ameonesha kutokubaliana na sera hiyo ya chama chake za zamani .
Akiwahutubia wanchi wa eneo la Sangamwalugesha, Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, John Shibuda amesema mfumo wa majimbo ni rahisi kuleta mafarakano.
“Kuna watu wanaonadi sera za majimbo, mimi sikubaliani kabisa na sera hizo kwani zikiruhusiwa zitawagawa Watanzania na kuleta ubaguzi wa kikanda na ukabila unaoweza kuleta mifarakano na kugombania rasilimali,” alisema Shibuda.
Aidha Shibuda amemsifu Rais Dk. John Magufuli, akidai kasimamia nidhamu kwa watumishi serikalini na kupambana na ufisadi.
Hii ni mara ya kwanza kwa John Shibuda kugombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri wa Mungano wa Tanzania .