Uongozi wa Yanga umepanga kuachana na wachezaji wao wa kigeni watano kutokana na viwango vyao ambavyo wameonyesha msimu huu.

Katika orodha hiyo ya wachezaji wa kigeni ambao wataachana nao yupo kipa Farouk Shikhalo ambaye amekuwa si chaguo la kwanza.

Meneja wa Metacha, Jemedar Said alisema kuwa kwa nyakati tofauti alizungumza na viongozi wa Yanga, Gharib Said, Senzo Mazingisa na Haji Mfikirwa.

“Wote kwa pamoja wameonyesha nia ya kumuongezea mkataba mpya Metacha na walinambia mwanzoni mwa mwezi wa sita watamsainisha mkataba mwingine” alisema Kazumari.

Inaelezwa kuwa tayari miamba ya soka ya Kenya, Gor Mahia imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya Shikhalo.

Yanga SC: Hatuutambui mchezo wa Julai 03
Aweso: Mradi ukabidhiwe ifikapo Juni 30