Shishi hana utani na maamuzi yake kwenye mapenzi, akipenda anapenda kweli lakini akiacha analigueza penzi kuwa kuwa….!

Mwimbaji huyo wa Bongo Flava ameuvuruga mpango wa waandaaji wa kipindi cha D’Weekend cha Clouds TV baada ya kugeuka mbogo akiwa studio mara tu baada ya kumuona mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda ambaye tangu waachane inaonekana madonda ya maumivu kati yao bado hayajapona.

Kupitia tangazo la kipindi cha D’Weekend, Shilole anaonekana akisimama ghafla na kulazimisha kuondoka akiwa amejaa hasira ndani ya studio hizo punde baada ya kumuona Nuh Mziwanda akiingia ndani ya studio.

Hata hivyo,  bado tatoo ya Shilole itabaki kwenye mwili wa Nuh Mziwanda ambaye alifahamika zaidi katika muziki wake baada ya kuanzisha uhusiano na mrembo huyo kutoka Igunga.

Maajabu ya Christmas: Taswira ya mtu akitembea juu ya mawingu yazua gumzo
Kim Poulsen Yu Njiani Kurejea Katika Soka La Bongo