Aliyekuwa Rais wa tisa wa Israel  Shimon Perez  amekimbizwa hospitali iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa Tel Aviv baada ya kuugua kiharusi.

Taarifa kutoka ofisi yake zimesema kuwa Perez anapumua kwa msaada wa kutumia kifaa maalumu.

Mwezi Januari mwaka huu Perez alifanyiwa upasuaji mdogo wa moyo baada ya kuugua mshituko wa moyo.

Mshindi huyo wa tuzo ya nobel ametimiza umri wa miaka 93 mwezi uliopita na amewahi kushikilia nyadhifa za juu zaidi katika serikali ya Israel,alimariza muda wake wa urais mwaka 2004.

 

Ligi Ya Mabingwa Ulaya UEFA Yaanza Kutimua Vumbi
Mrema Awapongeza Ukawa